Ezekiel 16:9-13

9 a“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta. 10 bNikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa. 11 cNikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako, 12 dnikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako. 13 eKwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia.
Copyright information for SwhKC